• Post detail
  • EAC yaahirisha mikutano yote kuhusu virusi vya corona
angle-left EAC yaahirisha mikutano yote kuhusu virusi vya corona

EAC yaahirisha mikutano yote kuhusu virusi vya corona

Jumuiya ya Afrika Mashariki imesitisha mikutano yote iliyopangwa hadi itakapotangazwa tena kutokana na mlipuko wa virusi vya corona duniani (COVID-19).

14 Mar 2020 - 00:00:00
Jumuiya ya Afrika Mashariki imesitisha mikutano yote iliyopangwa hadi itakapotangazwa tena kutokana na mlipuko wa virusi vya corona duniani (COVID-19). Ni baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC Vincent Biruta, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda kumwandikia Katibu Mkuu wa EAC, Liberat Mfumukeko, akitaka kuahirishwa kwa mikutano yote ya EAC inayohitaji umati mkubwa wa watu. Kwa hiyo, mikutano kadhaa iliyokuwa imepangwa kufanyika siku za usoni imesitishwa, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa 21 wa wakuu wa EAC utakaofanyika Machi, Baraza la 40 la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliopangwa kufanyika Aprili 14 na mikutano mingine mingi imeathiriwa na Maagizo hayo.

Picha

00