• Post detail
  • Fursa ya kushiriki katika Shindano la Mpango wa Biashara katika Kukabiliana na COVID-19
angle-left Fursa ya kushiriki katika Shindano la Mpango wa Biashara katika Kukabiliana na COVID-19

Fursa ya kushiriki katika Shindano la Mpango wa Biashara katika Kukabiliana na COVID-19

Serikali ya Japani iko tayari kukufadhili hadi USD 30,000 ili kutekeleza ubunifu wako.

17 Jul 2020 - 00:00:00
Je, una bidhaa au huduma bunifu zinazoweza kukabili janga la COVID-19 na jumuiya ya baada ya janga la COVID-19 AU una mpango wa biashara unaowezekana wa kuunda mifano (MVP)? Serikali ya Japani, kupitia shindano la Next Innovation with Japan (NINJA) iko tayari kukufadhili hadi USD 30,000 ili kutekeleza ubunifu wako. Makataa ya kupokea maombi ni tarehe 29 Julai, 2020. Maombi yatakaguliwa kulingana na mpangilio ambayo yalipokelewa - njo kwanza. Waombaji watazingatiwa kutoka: Angola, Burkina Faso, Botswana, Cameroon, Côte d'Ivoire, Misri, Ethiopia, Ghana, Kenya, Madagascar, Mauritius, Nigeria, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Tanzania, Tunisia, Uganda na Zambia. Tazama maelezo katika kiungo kilicho hapa chini kilichoandikwa kama shindano la mpango wa biashara:

Picha

Viungo

00