• Kenya
  • Rasilimali
  • Kujenga Uwezo
  • Mafunzo ya Biashara
  • Mafunzo ya Biashara

Mwongozo wa habari wa haraka

Kulingana na Fanikisha Initiative , mafunzo ya biashara kwa wafanyabiashara wanawake yanaongoza:

  • Kuimarishwa kwa matarajio ya wanawake kusonga mbele na kufaulu katika juhudi zao.
  • Kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika ngazi za kufanya maamuzi ambayo ni uwezeshaji wa rasilimali.
  • Kuongezeka kwa ufahamu katika ngazi ya biashara, serikali na jamii ili kuimarisha uwezeshaji wa wanawake.
  • Kuongezeka kwa uwezo na motisha ya wanawake kuchukua majukumu mapya na yenye changamoto katika viwango vya juu pamoja na bidii ya kufanya kazi kwa njia ya kuridhisha.
  • Uundaji wa mifano ya kuigwa ambayo wanawake wengine huitazama kwa minajili ya viwango na maendeleo/malengo ya ukuaji.

Mafunzo ya Biashara nchini Kenya

Madhumuni ya mafunzo ya biashara ni kuboresha utendaji wa biashara kwa biashara zinazoendeshwa na wanawake. Hii ina maana kwamba

SME zinazoongozwa na wanawake huwa na faida zaidi na kuathiri ubora wa maisha sio tu kwa wanawake lakini familia zao pia kutokana na upatikanaji wa mapato ya juu ya matumizi.
Mashirika mengi nchini Kenya yanawekeza katika kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake ili kusaidia kutatua suala la kutofanya kazi vizuri kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake, hasa kutokana na upatikanaji mdogo wa mtaji na ukosefu wa ujuzi.
angle-left Uweza Foundation

Uweza Foundation

Maelezo

Uweza Foundation inafanya kazi Kibera, Nairobi, Kenya. Uweza iliyoanzishwa mwaka wa 2008, inawapa watoto na vijana wa Kenya fursa za kipekee za kufuata njia ya maisha bora ya baadaye kupitia ugunduzi na ukuzaji wa vipaji na uwezo wao hivyo basi kupata elimu na hatimaye kupata mapato ambayo yanatumia uwezo wao wa asili.

Soma zaidi;

Maelezo ya mawasiliano

Uweza Foundation Mbali ya Barabara ya Karanja, ng'ambo ya St. Mary's Clinic, Kibera
POBox 21182-00505,
Nairobi-Kenya
Simu: +254 714 371964

Barua pepe; nbspnbsp

Tovuti;

Mipango ya Mafunzo

Mafunzo ya Biashara na Fedha- Kupitia mpango wa Bright Futures, Uweza huwa na vipindi vya mafunzo ya biashara na fedha. Mada za mafunzo hayo ni pamoja na ujasiriamali, kuzalisha wazo la biashara, masoko, utafiti wa soko, utunzaji wa kumbukumbu na mawazo ya akiba na mikopo ya vikundi. Washiriki pia wanafundishwa jinsi ya kuunda mpango wa biashara na pendekezo la biashara.

Soma zaidi;

Huduma za ziada za manufaa kwa wajasiriamali wanawake

Akiba na Mikopo ya Kikundi- Wanakikundi hushiriki katika mpango wa kuweka akiba wa quotmerry-go-roundquot, ambapo kila wanakikundi huchangia kiasi kidogo kila wiki na kisha wanakikundi wote hupokea zamu kupeleka jumla ya kiasi hicho nyumbani.

Shughuli za Kuongeza Kipato- Wanachama wa Bright Futures wamechukua jukumu la kusafisha Kituo cha Jamii cha Uweza na kufua jezi kutoka kwa programu ya Uweza ya Soka mara mbili kwa wiki, ili wapate mapato ya uhakika. Pia wameanzisha biashara ya kutengeneza sabuni ya maji ya kikundi ambapo wanatengeneza na kuuza sabuni hiyo wakiwa kikundi na kugawana mapato.

Mafunzo ya Stadi za Maisha- Wanakikundi hushiriki katika kipindi cha mafunzo ya stadi za maisha mara moja kwa mwezi kwenye mikutano yao juu ya mada zinazohusiana na kuwa msichana na mama mdogo huko Kibera, mara nyingi huongozwa na mwezeshaji kutoka nje. Mada za majadiliano ni pamoja na upangaji uzazi, afya na lishe ya mtoto, VVU/UKIMWI, na umuhimu wa elimu kwa watoto. Wanakikundi pia hushiriki katika vipindi vya mafunzo ya kompyuta katika maabara ya kompyuta ya kituo cha Uweza.